About me

My photo
I'm a man of God, full of his glory committed to serve him all the rest of my life. I'm working as an evangelist and a gospel musician.im here to enable ministers to meet the work field and gospel singer networking. you are all welcome to share anything for the glory of the mighty God

Saturday, August 13, 2011

JESUS CAN MINSTRIES

JESUS CAN MINISTRIES

JESUS CAN MINISTRIES

AKUNA LISILO WEZEKANA KWA MUMNGU  
MUNGU MKUU SANA

JESUS CAN MINISTRY
J.C.M

PROJECT
2011-212

LUBUMBASHI D.R. CONGO

JESUS CAN MINISTRY

Jesus Can Ministry ni muungano wa watu wachache wamcha Mungu, waimbaji katika huduma ya kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji na sio uimbaji tuu bali kueneza habari njema ya Kristo Yesu ulimwenguni, tajumuika pamoja na kuifanya huduma hii kuwa na nguvu zaidi.

Kupitia Ufunuo wa Roho mtakatifu, tumepata maono hiii ili kulisaidia taifa ambalo ni ndugu zetu walio katika mazingira magumu ya maisha.

Tupo Dar es Salaam ambapo ni sasa makao makuu ya Ministry hii na tunazidi na tutazidi kuwafikiria wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na majanga mbalimbali. Mara tukapewa maono na mzigo huu wa kusaidia kwa njia hii ya huduma tuliyo nayo; bila shaka mioyo yetu imethibitika kuwa tunaweza.

Kulingana na maisha halisi ya siku hizi, mzunguko wa maisha sio rahisi wala sio sawa kwa watu wote, kwasababu watu wapo katika rika mbalimbali na hali tofauti, bali kutokana na maono tuliyonayo kwa ajili ya vijana katika kuwakomboa kiuchumi, kimaisha, kifikra na kiroho.

Jesus Can Ministry ni huduma ambayo inahusika na vijana kwa kuwafundisha maadili mema, pia kuwakomboa katika majanga mbalimbali kama vile umaskini, maradhi mbalimbali (Ukimwi, TB), madawa ya kulevya na vilevile ni kikundi ambacho kina tamani kuchangia kwa kuwasikiliza wanyonge na kuwainua na kuwasaidia kadri ya uwezo wetu. Ikiwepo kuwatetea watoto yatima na Wajane. Tumeshuhudia huduma nyingi zinazo wasaidia  watu hawa zina nguvu na zimebarikiwa sana ni mfano wa kanisa letu kwa hapa TANZANIA CALVARY TABERNACLE CHURCH inayoongozwa na mtumishi wa Mungu BISHOP SAMUEL MOMA NKAMPINGA amekuwa akiwasaidia sana wajane na mayatima ndio siri ya mafanikio ya huduma hiyo na baba ametuambukiza hali hiyo. Pia kuwasaidia kiuchumi na wale watu wasiojiweza, walioko mahospitalini na katika mazingira kwa kuwatia moyo na kuwapa matumaini.

MAELEZO
          Katika maono haya tumepanga kufanya mashindano ya waimbaji wote wa mkoa wa LUBUMBASHI ambao ni kwaya na waimbaji binafsi kutoka kila sehemu ya mkoa huo.

Katika kila mkoa tutakusanya kwaya mbalimbali na waimbaji binafsi ambapo watajiandikisha kwa ajili ya mashindano hayo. Kwa taarifa tulionayo ni kuwa zipo kwaya zisizopungua 400 katika kila sehemu ya mkoa huo inayolengwa ya mashindano hayo.

Kila sehemu itawakilisha vikundi 100 ili kuingia katika mashindano ya kuwatafuta washindi watatu (3) kwa sababu hii tutakuwa na matamasha yasiyozidi kumi na nne (14) ili kukamilisha zoezi la kuwapata (4) bora watakaofuzu mashindano ya mwisho ya kupata kwaya na waimbaji binafsi bora zaidi.

Kwa ajili ya jambo hili tunahitaji kuwaalika wasanii maarufu atakaye kuja kuzindua tamasha hili kubwa litakalo watafuta watatu (3) bora na kuwatunukia zawadi kem kem. Sasa kwa washindi wetu kama ilivyo makubaliano ya baraza, atapatikana wa kwanza, pili, tatu na wa nne kila nafasi ya kwaya na muimbaji binafsi atapata zawadi yake kulingana na nafasi atakayopata.

UTARATIBU WA ZAWADI
WA KWANZA
WA PILI
WA TATU
WA NNE
> Gari aina ya NOAH VOGXY
> 2000 USDS
> 1000 USDS
> 500 USDS
> Video Recording
> Video Recording
> Video Recording
> Video Recording
> Audio Recording
> Audio Recording
> Audio Recording
> Audio Recording

MALENGO YA KIUCHUMI:

Kama ilivyo utaratibu wa kazi hii; tunatarajia kulipisha kila tamasha kiasi kisichozidi 3$ kwa viti vya watu wote na viti maalum itakuwa kuanzia 10$ jumla ya fedha zitakazo patikana tutatumia asilimia hamsini na tano (55%) kwa ajili ya kuendeleza kazi. Asilimia 25% itaenda katika mfuko wa zawadi na asilimia 20% itaenda katika mfuko wa kuwasaidia familia, watu waliokumbwa na majanga na mikasa mbalimbali, pia bila kuwasahau ndugu zetu wajane na watoto yatima.

MADHUMUNI YA HUDUMA HII

          Madhumuni ya Kazi hii ni kuwasaidia wajane, yatima, wasiojiweza na pia kukuza vipaji vya wanamuziki na wasanii mbalimbali walio katika hali ngumu.

Vile vile kuwaelimisha vijana na kuwapa na kuwaongoza katika fursa za kazi na kujitegemea. Kwa kuwapatia matumaini na ukarimu huu ndio utakao uleta ulimwengu pamoja na kuzimaliza tofauti nyingi baina ya hali ya maisha au mzunguko wa maisha wa wananchi wa mkoa wa LUBUMBASHI kwa maana:- “UKIMPENDA MWENZIO HUTAMUUMIZA KWA LOLOTE”.

          Msaada huu utawawezesha kumudu mahitaji yao kwa vitu mbalimbali wa hali na mali kama vile chakula, mavazi na makazi ya kudumu. Tunatarajia kusaidia familia zisizopungua 250 kwa takribani watu 3600 watafaidika na huduma hii.

USALAMA

Ili kuhakikisha kwamba msaada huu umewafikia watu wanaostahili, tutaandaa kamati maalum itakayoshughulikia mambo hayo hadi mwisho.

KUJIANDIKISHA

Kila kikundi kitajiandikisha kwa kiasi cha 20 USD. Kutakuwa na fomu ya kujaza ili kufanya makubaliano baina yetu

MAPENDEKEZO
1.   OFISI
Ofisi ya mradi huu iandaliwe, yenye vifaa kama computer ili kutuwezesha kupata maandishi yote tutakayohitaji wakati wa zoezi hili.

2.   KAMATI
Mradi huu unahitaji kuwa na kamati ili kuwezesha maendeleo ya huduma hii kuwa dhahiri na kutekelezeka.

3.   WARSHA (PRESS CONFERENCE)
Ili kuwezesha kazi hii kufaulu vizuri inabidi kuwe na matangazo kwenye vyombo vya habari yaani radio, televisheni, vipeperushi na kwenye mabango, matangazo makanisani huku tukijadiliana na watangazaji, ni lazima matangazo iwafikie walengwa na kuhakikisha kwamba waalikwa wetu wanahusika katika mradi huu.

Bila kusahau kutakuwa na judges watakaofuatilia kwa kina zaidi hali ya waimbaji, kulingana na ujuzi na uzoefu wa kazi yao watawachagua waimbaji kulingana na vipimo, mpaka pale watakapompata mshindi wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne. Pia jambo hili lifuatiliwe na kuzingatiwa bila rushwa wala upendeleo kuingilia kati na ingekuwa bora na kuna umuhimu wa judges kumjua, na kumcha Mungu kwa uaminifu na uadilifu.

4.   WAFADHILI (SPONSORS)
Kuna uhitaji na umuhimu mkubwa sana wa kuwa na wafadhili watakaoguswa na huduma hii kikamilifu kutoka mioyoni mwao wala sio mioyo ya kubahatisha kwa chanzo cha kupata fedha kupitia huduma hii bali kulitukuza jina la Yesu Kristo kwa kuwasaidia, kuwainua na kuwapa tumaini vijana, wajane, yatima na wasiojiweza. Ili kutuwezesha kufikia malengo yetu. Huduma hii itahakikisha inawatangazia wadhamini wetu biashara zao kitaifa na kimataifa. Pia tunahitaji kuwa na watu ambao ni waombaji watakaoungana na kanisa letu la Tanzania Calvary Tabernacle Church iliyoko Dar es Salaam - Tanzania, ili kuibeba maono haya kwa maombi mpaka mwisho.

5.   MAZINGIRA
Hili ni jambo kuu na la muhimu sana kuwa kupata nafasi kubwa, nzuri tutakayoweza kufanyia tamasha hili, sehemu itakayoweza kuweka watu wote watakaohudhuria ipasavyo na pia kuhakikisha kila mahali pameridhia.

6.   VYOMBO VYA MUZIKI
Katika kila eneo/sehemu ya mkoa wa LUBUMBASHI inabidi tuangalie uwezekano wa kupata vyombo vizuri, vizima, vitakavyokidhi mahitaji yetu kwa ajili ya kukamilisha zoezi hili liende vizuri na sawasawa na madhumuni mahsusi ya huduma hii.

OMBI LETU
 Kwa mujibu wa kusaidia ndugu walioko katika shida, na mazingira magumu kwa kuishi maisha magumu, kutokana na maradhi, majanga mbalimbali na umaskini. Kila mtu atakayeguswa na jambo hili kwa moyo wake mwema au idara yoyote ya maendeleo, kampuni au shirika binafsi, kutuunga mkono kwa kuchangia kwa hali na mali ili kutuwezesha kufikia malengo yetu. Na Mungu wa Mbinguni atabariki maisha yako.

Malaki 3:106

Ø  “Mkinijaribia kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungilia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la”.

Ø  Husika na mambo ya Mungu na Mungu atahusika na mambo ya maisha yako.

DAR ES SALAAM TANZANIA

BENN CHRISTOPHER
PROJECT MANAGER