Warumi 8: 31-39
Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayewashtaki wateule we Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ninani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yupo mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauwawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kama kondoo wa kuchijwa. Lakini katika mambo hayo tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala yaliyopo, wala yatakayo kuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika kristo Yesu Bwana wetu.
No comments:
Post a Comment